“Chombo cha kudhibiti upandaji holela wa bei kwenye sekta ya Afya kuanzishwa”- Dk.Kigwangalla

“Chombo cha kudhibiti upandaji holela wa bei kwenye sekta ya Afya kuanzishwa”- Dk.Kigwangalla

Serikali inaangalia uwezekano wa kuanzisha chombo maalumu cha kudhibiti gharama na bei zinazotozwa na vituo vya huduma za afya, ikiwa ni pamoja na bei za dawa na vifaa tiba.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk. Hamisi Kigwangalla alisema bungeni kuwa mbali na mkakati huo, wanashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa mkakati wa kuongeza uzalishaji wa dawa nchini ili kukidhi angalau asilimia 60 ya mahitaji katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla amebainisha kuwa, mbali na mkakati huo, wanashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa mkakati wa kuongeza uzalishaji wa dawa nchini ili kukidhi angalau asilimia 60 ya mahitaji katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akijibu swali la msingi la mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia aliyetaka kujua kama kuna mpango wa kuanzisha chombo cha kudhibiti bei kubwa za dawa binadamu nchini, Kigwangalla alisema gharama hizo hupanda kutokana na kutegemea zaidi dawa kutoka nje ya nchi na huathiriwa na kushuka kwa thamani ya shilingi.

“Kwa sasa bado tupo kwenye mchakato wa kutazama ni chombo cha muundo gani, majukumu gani na kitaendeshwa vipi. Hata nchi nyingine zilizoendelea zina chombo kama hicho,” alisema Dk. Kigwangalla.

Hata hivyo chombo hicho bado  hakijaanzishwa na Wizara yake ya Afya ipo mbioni kufanya hivyo kwa sasa ili kumuondolea ‘mzigo’ mwananchi ambaye anapewa gharama kubwa katika matibabu yake.