Naibu Waziri wa Afya azindua duka la MSD Arusha

Naibu Waziri wa Afya azindua duka la MSD Arusha

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuacha kuhujumu dawa zinazopelekwa kwa ajili ya wananchi na si za biashara kama wanavyofanya, onyo hilo yamesemwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Dkt.Hamisi Kigwangwalla wakati akiongea na wafanyakazi wa bohari ya dawa (MSD) pamoja na wale wa hospitali ya mkoa ya Mount Meru. Dkt. Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano yenye kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”haitawavumilia watumishi wa aina hiyo na kama wapo basi waanze kujipima kabla rungu la dola halijawafikia. Aidha,alisema suala la upatikanaji wa dawa kwa wananchi na kwa bei nafuu ni moja ya mambo yaliyopewa kipaumbele katika serikali ya awamu ya tano
“Wananchi wanatakiwa kupata dawa sahihi,kwa bei nafuu na kwa wakati,ndo maana serikali imeamua kufungua maduka ya dawa ya ndani ya hospitali,Hii ni moja ya malengo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha Malibu”
Hatahivyo aliongeza kuwa katika kudhibiti upotevu wa draws nchini,serikali imeanza kutekeleza uwekaji nembo ya GoT katika vidonge vyote”na mimi nawapa changamoto ya kuweka mkakati wa kuweka rangi Maalum ‘colour code’
Kwa dawa zote zinazokuwa.zimenunuliwa na serikali,sambamba na huo mkakati wenu wa nembo

Licha ya hivyo aliwataka wakuu wa hospitali,vituo vya afya pamoja na zahanati wasipokee dawa bila kuwepo kwa kamati ya afya ambayo ndio wawakilishi wa wananchi wa mahali husika ili kusiwepo na udanganyifu na kwenda kwenye mfumo usio rasmi pamoja na kuzibandika dawa zilizopokelewa kwenye mbao za matangazo
Aliitaka bohari ya dawa (MSD) kukamilisha uwekaji nembo dawa zilizosalia na wawe na utaratibu wa kusimamia na kukagua kama dawa za serikali zimefika hadi sasa vidonge vipatavyo 65 vimekwishawekewa nembo ya GoT.
msd-arusha1
Baadhi ya wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)kanda ya kaskazini wakimsikiliza naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.
msd-arusha2
Watumishi wa hospitali ya mkoa ya mount Meru wakimsikiliza kwa makini Dkt.Hamis Kigwangwala.
msd-arusha3
Naibu waziri Dkt.Hamisi Kigwangwala akiongea na watumishi hao.
msd-arusha4
Watumishi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya naibu waziri wao.